Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Ayatullah Nasir Makarim Shiraz alisema siku ya Jumapili katika Haran ya Sayyidat Fatima Maasuma Qum; Kazi ya Mawahabi ni kutuhumu Mashia kuwa wao wadai kuwa Qurani ni pungufu yaani kuna baadhi ya Aya za Quarani zimeongezwa na zengine kufutwa, maneno hayo tuhuma na urongo kwa Mashia, Mashia hawaitakidi kubadilishwa Qurani au kupunguzwa na kuongezwa baadhi ya Aya.
Akiendelea kusema: Qurani ni Muujiza wa milele kamwe hawezi mtu kubadili au kuongeza maneno katika Qurani kwani wengi walijaribu hawakuweza hivyo, na itikadi ya Wanazuoni wote wa Kishia ni hiyo.
Ayatollah Makarim Shiraz: Alipoanga Dunia Mtume(saw) aliacha vizito viwili na vyo ni Qurani na Ahlul Bayt(as), na wafuasi wa Nyumba ya Mtume(saw) wajifaharisha kwa vizito hivyo.
Aidha alisema: Surat Al-Ahzab ni moja mwa Sura za Qurani ni lazima wafuasi wa Ahlul Bayt(as) wajifunze na kufunzana Sura hii hasa kwa wanafamilia kwani kusoma Sura hii kunafadhila nyingi, pia usomaji Sura hii hupunguza Adhabu ya Kaburini.